<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>63</hymn_number>
<lyrics>[V1]
 Ndugu wa kirohoni
 Mliokombolewa,
 Tafakarini sana
 Yatupasayo.

[V2]
 Wapenzi wake Yesu
 Tuliokombolewa
 Tujitoe kabisa
 Wengi waponywe.

[V3]
 Siku itatimia
 Tutakapoulizwa
 Wale wa nyumba zetu
 Na majirani

[V4]
 Tujitoeni, ndugu,
 Tukahubiri Injili.
 Atutumie Roho
 kuponya wengi.

[V5]
 Wasiokombolewa
 Ni wengi vijijini,
 Wataokolewaje
 Tukiogopa?

[V6]
 Bwana alijitoa
 Akapotewa mengi,
 Ili atuokoe,
 Tusiwe waoga.

[V7]
 Aliyetununua,
 Kwa kuimwaga damu,
 Angalieni sana
 Msimwepuke.</lyrics>
<title>Ndugu Wa Kirohoni TZR63</title>
</song>